Uzinduzi wa tuzo za kwanza kabisa nchini Tanzania ijulikanayo kama 'Tanzania Gives Back'.
Malengo ya tuzo hizi ni kuonyesha mchango mkubwa wa watanzania na wasaidizi wenye utaalam kutoka nje ya nchi wanaojitolea katika jamii kwa kutoa muda na ujuzi wao kwa ajili ya kuendeleza jamii.
Kuna mashujaa wengi wasiotajwa katika Tanzania na bado mara nyingi dhana ya kujitolea inahusishwa na wafadhili au wajibu mashirika kwenye taratibu zao kwa jamii. Katika hali halisi, kuna watanzania ambao hutoa muda na ujuzi wao wa thamani kwakuchangia mabadiliko chanya bila malipo ya fedha.
Unamjua mtu ambaye husaidia watu wengine katika jamii? Mtu ambaye anatumia muda wake bila malipo kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wengine? Tunataka kusikia zaidi juu ya watu hawa na wewe unaweza kutusaidia kufafanua juu ya shughuli na msaada wao kwa jamii na kuwateua kwa ajili ya tuzo za Tanzania Gives Back 2011.
Mwaka huu vipengele 8 katika Tanzania Gives Back vitashindwanishwa katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru kwa kuwatangaza mashujaa hawa kutoka kote Tanzania. Jaza kikamilifu fomu ya uteuzi kabla ya Mei 23, 2011 na kutuambia juu ya mtu ambaye unaemfahamu alietoa mchango mkubwa kwa manufaa ya watu wengine.
Vipengele vya uteuzi:
- Afya na Ustawi wa Jamii
- Elimu na Mafunzo ya Ufundi
- Walemavu
- Mazingira
- Watoto na Vijana
- Kupunguza Umaskini na Biashara ndani ya Jamii
- Uwezeshaji wa kijinsia
- Utamaduni
Follow the link to www.jitoleetanzania.com to complete the nomination form.
Pata fomu ya Uteuzi kwa Kiingereza na Kiswahili chini.
![]() |
| Tanzania Gives Back is proudly Supported by the European Union. |
![]() |
| Tanzania Gives Back is proudly Sponsored by Sumaria. |





